MKOA WA KATAVI WAREJESHA MIL.56 ZA WATUMISHI HEWA



Mkoa wa Katavi umefanikiwa Kurejesha fedha za watumishi hewa kwa asilimia 23.34 ambapo ni  kiasi cha zaidi ya shilingi  milioni 56  kati ya  milioni  zaidi ya 240 zimelipwa kama mishahara hewa.

Akitoa Taarifa hiyo  kwa Waandishi wa Habari Ofisini Kwake Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali  mstaafu  Raphael Muhuga amesema  kuwa halimashauri zote nne za mkoa wa katavi zimerejesha fedha hizo japo bado hazijakamilika .
Muhuga  ametoa Ufafanuzi juu ya watumishi hao waliokuwa wakiendelea kulipwa fedha kuwa ni pamoja na watumishi waliokuwa na Vyeti vya kugushi  waastaafu watumishi walifariki ambapo baada ya kuunda  timu ya  kuanza uchunguzi  wengine walikimbia na kutokomea kusikojulikana.
Hata hivyo  Muhuga amesema Utaratibu wa kurejesha fedha zote zilizoibiwa unaendelea katika Halmashauri zote na kudai kuwa utaratibu huo ukikamilika hatua kali zitachukuliwa kwa maafisa utumishi katika halimashauri zote nne  walioisababishia hasara serikali .

Fedha  hizo  zimerejeshwa  kufuatia  agizo lililotolewa  na  Mkuu wa  Mkoa  wa  Katavi   Meja  Jenerali  Mstaafu  Raphael  Muhuga alilolitowa   kwa  Wakurugenzi wote wa  Halmashauri za  Mkoa wa  Katavi  la  kuwataka wahakikishe   fedha  zote  walizolipwa  watumishi  hewa   46  waliobainika   katika  Mkoa wa  Katavi zinarejeshwa  Serikalini .
Mkuu wa Mkoa mapema Mwezi Aprili alikuwa amesema   hadi  kufikia   Mei  4  mwaka  huu   Mkoa  wa  Katavi ulikuwa  na  idadi ya  watumishi  hewa   46 ambao  walibainika  wakiendelea  kuchukua  mishahara  wakati hawasitahili  kulipwa na kuitia   hasa   Serikali  kiasi  cha   shilingi Milioni  200,792,448.
Katika katika taarifa ya mwezi Aprili mwaka huu, Halmashauri ya  Wilaya  ya  Mpanda walibainika  watumishi  hewa  tisa      na wamerejesha  kiasi  cha  shilingi milioni 12,674,201  kati ya  shilingi   milioni  33,759,041  na  Halmashauri  ya Wilaya  ya  Mlele  yenye  watumishi hewa    tisa  wamerejesha  kiasi  cha  shilingi  milioni 9,280,000  kati ya   shilingi  milioni   46,031,120.
Meja   Jenerali  Mstaafu  Muhuga  alisema  Manispaa ya   Mpanda   ambayo ilibainika kuwa na     idadi ya  watumishi  hewa 16   hadi  june  20 ilikuwa  imerejesha  kiasi   cha   shilingi   Milioni 24,841,899 kati ya  Tsh 69,917216, Halmashauri  ya  Nsimbo  yenye  watumishi  hewa 11  hadi  sasa  imerudisha   Tsh mil.9,306,800  kati ya  Tsh  90,661,880.
Kiasi hicho cha Zaidi ya Shilingi milioni 240 kinahusisha sekta mbalimbali zikiwemo Elimu na afya huku watumishi wengine wakihusishwa kughushi vyeti.
Halmshauri za Wilaya nne ambazo zinahusishwa katika suala la watumishi hewa ni pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda,Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda,Nsimbo na Mlele
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo 
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA