WAZIRI NAPE AFUTA KAREFA,AMWAGIZA KATIBU TAWALA KUSIMAMIA UCHAGUZI WA VIONGOZI UPYA



Na.Issack Gerald-Katavi
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemuagiza katibu tawala wa mkoa wa Katavi Bw Paul Chagonja kufuta uongozi wa mpira wa miguu KAREFA na kusimamia zoezi la uchaguzi wa viongozi wapya baada ya kufuta uliokuwepo.

Kiongozi huyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa huo amewasili jana mjini mpanda majira ya saa 9 mchana akitokea mkoani Rukwa.
Aidha ameahidi ukarabati wa uwanja wa mpira wa miguu utakao endana na hadhi ya mkoa.
Waziri Nauye mara baada ya kuwasili jana Mkoani Katavi akitokea Mkoani Rukwa,amezungumza na wadau mbalimbali wa habari utamaduni sanaa na michezo ikiwemo viongozi wa serikali ya mkoa wa Katavi katika ukumbi wa idara ya maji mjini mpanda.
Amesema lengo la ziara yake katika mikoa mbalimbali ikiwemo mkoani ni kutaka kuishusha wizara yake mikoani ili kutekeleza majukumu ya wizara hiyo kiurahisi.
Waziri Nape leo anatarajia kuondoka mkoani Katavikuelekea mkoani Kigoma ambako ataenda mpaka mkoani kagera katika ratiba yake ya kufanya ziara katika mikoa ya pembezoni mwa nchi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA