MTOTO MWENYE ULEMAVU WA VIUNGO ATUNZWA NDANI YA NYUMBA MIAKA MIWILI BILA HATA YA KUPATA MAHITAJI YA MSINGI
Na.Issack Gerald-Katavi
Taarifa
iliyopatikana Aprili mosi mwaka huu ni yan mtoto mmoja mwenye ulemavu wa viungo katika manispaa ya Mpanda mkoani katavi ambaye
amekuwa akifungiwa ndani kwa muda wa miaka miwili na kukosa haki zake za
msingi kama elimu wakati mwingine hata chakula.
Akithibitisha
kuwepo kwa tukio hilo mama mlezi wa mtoto
Bi Ester Kapandila amesema baba mzazi ndiyo chanzo cha tatizo hilo.
Kutokana
na tatizo la mtoto huyo,dada yake aitwaye Christina Mziyuka ambaye ni yeye ni
mwanafunzi kwa ajili ya kumhudumia motto huyo.
Mtoto
Christina ambaye awali alikuwa akisoma darasa la sita katika shule ya Msingi
Mwenge iliyopo Sumbawanga Rukwa,amesema kuwa mama huyo mlezi aliyekuwa akimhudumia
mtoto huyo mlemavu baadaye alikatazwa na baba wa mtoto huyo mwenye ulemavu na
jukumu la matunzo kupewa dada yake mwanafunzi na kupelekea mwanafunzi kusitsha
masomo ili kumhudumia kaka yake.
Kwa
upande wake afisa ustawi wa jamii Bi
ledy Gunda amesema mtoto huyo amekuwa
akitengwa na kunyimwa fursa kama watoto wengine.
Aidha
ametoa wito kwa jamii kutambua haki ya mtoto na kushilikisha vyombo
vya kijaamii kwa ajili ya msaada zaidi.
Comments