MKUU WA WIALAYA YA MPANDA AAGIZA ARDHI YA HEKTA 45 ILIYOUZWA NA UONGOZI WA KIJIJI KINYUME CHA SHERIA KWA MWEKEZAJI KUREJESHWA KWA WANANCHI
KATIKA kutatua Migogoro ya aridhi nchini Serikali Wilayani
Mpanda imeagiza kurejeshwa kwa wananchi Mara Moja kwa eneo la hekta 45 liliuzwa
kinyume cha taratibu kwa mwekezaji Katika Kijiji cha Magamba.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw,Pazza
Mwamlima Katika Mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji hicho sambamba na
Kuagiza kukamatwa kwa mwenyeti wa kijiji hicho Bw,Andrea Petro Katuma ambaye
hata hivyo alimaliza Muda wake.
Katika Mgogoro huo imeleezwa kuwa Bw,Andrea Petro Katuma na wajumbe wake Katika
serikali ya Kijiji waliidhinisha Kuuzwa kwa eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 45
kwa Mwekezaji anayefahamika kwa jina la Lucia Paulo Shabani Mkazi wa Mpanda
Mjini kwa Kiasi cha shilingi Milioni 9
kwa Mkataba wa Miaka 99.
Katika hatua nyingine,baadhi ya wakazi wa
kata hiyo ya Magamba iliyopo manispaa ya Mpanda wameelezea kufurahishwa na
hatua mbali mbali zinazochukuliwa na Serikali
katika kuwawajibisha viongozi wasio waadilifu.
Wamesema
ukosefu wa maadili kwa viongozi wa umma na kufanya kazi kwa mazoea
kulilitumbukiza taifa katika wimbi la umaskini.
Sanjari
na hayo wakazi hao wameongeza kwa kusema kuwa zipo changamoto lukuki katika
serikali za mitaa ambazo ni kikwazo kwa maendeleo, ambazo zinapaswa kutatuliwa
wakitolea mfano wa migogoro ya ardhi na huduma ya afya.
Tangu
Rais Dr John Pombe Magufuri aingie madarakani kumekuwa na mageuzi makubwa
katika mfumo wa utawala hasa kusimamia uwajibikaji na uadilifu kwa lengo la
kuwaletea maendeleo wananchi.
Comments