WAGONJWA WAANZA KUTEMBEZA KICHAPO KWA WAUGUZI HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA
Na,Meshack Ngumba-Mpanda
KUFUATIA tukio la jana la Muuguzi Katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda Kupigwa
na Mgonjwa aliyekuwa akimuhudumia, Serikali imeshauriwa Kuimarisha Usalama wa
watumishi Katika maeneo yao ya Kazi.
Katika hali isiyo ya kawaida imezoeleka
kusikia wahuduma wa afya Katika vituo mbalimbali hapa nchini wakilalamikiwa na
wagonjwa Kwa Kutumia lugha zisizokuwa na staha,lakini safari hii hali imekuwa
tofauti Kufuatia tukio la Mgonjwa
Kumpiga ngumi Muuguzi wa zamu aliyekuwa akimuhudumia Kwa Madai ya Muuguzi
Kumtaka Mgojnwa huyo alale Kitanda Kimoja na Mgonjwa Mwenzake.
Bi Recho Matinya ni Muuguzi Katika
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambaye pia ndiye Mwathirika wa tukio hilo amesema
kuwa alipigwa ngumi,ambapo baada ya hali hii ilimlazimu Muuguzi huyu kuiomba
serikali Kukomesha Kadhia Kama hii Kutotokea kwa watumishi wengine wa umma na pia Katika sekta nyingine
Maria Komba ni shuhuda wa tukio hilo kwa
upande wake alilaani Kitendo hicho na kuitaka Serikali iangalia namna ya Kulinda haki za wauguzi akisema kuwa mgonjwa huyo aliamka katika kitanda na kumvagaa muuguzi.
Ni Kipindi cha Wiki Moja Kimepita
tangu wabunge wa Viti Maalumu Mh,Anna
Lupembe na Mh Taska Mbogo Kutembelea Hospitali hiyo ili Kujionea Mapungufu
yaliyopo lakini hata kabla hawajaingia ndani Kulitokea Mvutano Kuhusu uhalali
wa Kufungwa kwa geti la Kuingia Katika hospitali hiyo Muda wote.
Kutokana na tukio hilo la Mgonjwa Kumpigwa Muuguzi wakati akimuhudumia anazungumzia
ulazima wa Kufungwa kwa geti hilo.
Hivi karibuni waaguzi Mkoani Mwanza
walilazimika kugoma kufanya kazi wakishinikiza serikali kuingilia kati wakidai
kufanyiwa udhalilishaji ikiwemo kudia kuelekezwa majukumu na wagonjwa.
Comments