VIONGOZI STENDI KUU YA MABASI MANISPAA YA MPANDA WAMWANGUKIA MKUU MPYA WA MKOA KATAVI KUTATUA CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU INAYOWAKABILI,BARABARA KUTOKA MPANDA HADI TABORA BADO PASUA KICHWA
Uongozi wa Stendi kuu ya mabasi
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,umemwomba Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral
Raphael Muhuga kuingilia kati kutatua changamoto ya kutowaka kwa taa za umeme
katika stendi tangu mwaka jana pamoja na wasafiri kukosa mahali pa kujikinga
mvua na jua.
Ombi hilo limetolewa leo na
Mwenyekiti Msaidizi wa Stend Bw. Ramadhani Nkwizu wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sanjari na Mpanda
Radio Katika stendi hiyo.
Amesema licha ya Mkurugenzi wa
Manispaa ya Mpanda na Mkuu wa Wilaya Mpanda kuahidi kutatua changamoto hiyo
tangu mwaka jana,hakuna kilichotekelezeka mpaka sasa.
Kwa upande wake Jailos Kipenye
amesema kuwa watu wamehofia kuingiliwa na waharifu pamoja na kuibiwa mali zao
kutokana na kutokuwepo kwa mwanga nyakati za usiku.
Suala la barabara kutoka Mpanda
Kupitia Tabora ikiwa ni takribani miezi 3 sasa tangu katazo la kutumia barabara
hiyo kutumika kutolewa wasafirishaji na wasafiri wanakumbwa na adha ya kutofika
Tabora kwa muda mwafaka pamoja na
wasafiri kutumia kiasi kikubwa cha nauli.
Aidha viongozi hao wakamwomba mkuu wa
Mkoa kushughulikia tatizo la barabara inayoanzia Mpanda hadi Tabora.
Kufuatia hali ya sintofahamu juu ya
hatima ya barabara kutoka Mpanda Kuelekea Inyonga hadi Tabora,Machi 25 mwaka
huu,Mkuu wa Mkoa wa Katavi alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara
kutoka Mpanda Kuelekea Tabora aliitaka serikali ya Wilaya ya Mlele kuendelea
kuzuia magari makubwa yakiwemo ya abiria kutoruhusiwa kupita katika barabara
hiyo kwa kuwa msimu wa mvua za masika unaendelea isipokuwa akasema kuwa magari
madogo yasiyo ya abiria yanaruhusiwa kupita.
Mto Koga hupokea maji kutoka mito ya
Rungwa na Chunya kupitia ziwa Rukwa
Barabara ya kutoka Mpanda Katavi hadi
Tabora ilizuiliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk.Ibrahim Msengi
aliyezuia barabara hiyo kutumiwa na vyombo vya usafiri Januari 26 mwaka
2016,kutokana na daraja la mto Koga linalotenganisha Mkoa wa Katavi na Tabora kukatika
ambapo jumla ya watu 10 walikufa maji baada ya gari walilokuwa wakisafiria
kusombwa na maji.
Comments