UTEUZI WAKUU WA MIKOA RUKWA,KATAVI,KIGOMA NA KAGERA WANAJESHI WATUPU(KATIBU TAWALA NA MKUU WA MKOA KATAVI NI MAJENERALI WA JESHI)


Na.Issack Gerald
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli Machi 13 amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 wakiwemo 13 wapya na 13 waliokuwa katika serikali ya awamu ya nne ya serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
                                                      
Mkuu wa Mkoa wa Mpya wa Mkoa wa Katavi Jeneral Raphael Mugoya Muhuga(PICHA NA.Issack Gerald)
                                           
Jeneali Paul Chagonja Katibu Tawala Mpya Mkoa wa Katavi aliyeteuliwa Januari 29,2016 (PICHA NA.Issack Gerald)
                                                        
Paul Chagonja katibu Twala mpya Mkoa wa Katavi aliyeteuliwa Januari 29,2016 (PICHA NA.Issack Gerald)

Katikia Uteuzi huo wamo wanawake watano ambao ni,
Anna Malecela Kilango
Shinyanga
Amina Juma Masenza
Iringa
Halima Omary Dendegu
Mtwara
Dkt. Rehema Nchimbi
Njombe
Chiku Galawa
Songwe(Mkoa mpya)
Wakuu wa Mikoa waliotemwa ni Ludovick Mwananzila (Tabora), Fatuma Mwassa (Geita), Issa Machibya (Kigoma), Mwantumu Mahiza (Tanga), Parseko Kone (Singida) na Abbas Kandoro (Mbeya).
Wengine ni Magalula Saidi Magalula (Rukwa) Rajabu Rutengwe (Morogoro), Dk Ibrahim Msengi (Katavi), Asery Msangi (Mara), Elaston Mbwilo (Simiyu) na Ali Rufunga (Shinyanga).
Wakati huo huo wakuu wa Wilaya waliopandishwa kuwa mkuu wa Mkoa ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro huku Jordan Rugimbana akiteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma.
Pia aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Antony Mataka  sasa anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Zelothe Steven, amepandishwa na sasa anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. .
Katika Uteuzi mpya wa wakuu wa mikoa,umewapa nafasi wanajeshi wane kuwa wakuu wa mikoa.
Wanajeshi walioteuliwa kuwa Wakuu wa Mikoa wapya ni Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na Meja Jenerali mstaafu, Salum Kijuu anayekwenda Mkoa wa Kagera.
Majenerali wengine ni Meja Jenerali mstaafu, Raphael Muhuga anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Lakini Pia  aliyekuwa Naibu Waziri Kilimo, Ushirika na Chakula, Godfrey Zambi anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Wakuu wa mikoa walioendelea kwenye vituo vyao vya kazi ni Daudi Ntibenda (Arusha), Amina Masenza (Iringa), Joel Bendera (Manyara), Halima Dendegu (Mtwara), Dk Rehema Nchimbi (Njombe), Evarist Ndikilo (Pwani) na Said Mwambungu (Ruvuma).
Kwa ufupi ni kuwa Mkoa wa Katavi sasa unakuwa na viongozi wa ngazi za juu wawili ambao wamekuwa maafisa wa jeshi kwa kwa nyakati tofauti na maeneo mbalimbali.
Kama unakumbuka January 29, 2016,Rais wa Tanzania Rais Magufuli alimteua Kamishna wa polisi Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi ambako alijaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa ambapo huenda Bw.Kipande akawa miongoni mwa viongozi waliovunja rekodi ya kuwa katika kituo cha kazi kwa muda mfupi kama katibu tawala.
Huyu alikuwa amechukua nafasi ya Mhandisi Emmanuel Kalobelo aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu katika Mkoa wa Katavi tangu mwaka 2012 Katavi ilipopewa hadhi ya kuwa Mkoa.

Kabla ya Kamishna Paul Chagonja kuteuliwa Desemba 08 mwaka 2015 kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi,alikuwa Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania kitengo cah Zimamoto na uokoaji.

Hapo ilikuwa katika nafasi ya Katibu tawala Mkoa wa Katavi.

Katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mkoa wa Katavi sasa utakuwa na wakuu wa Mikoa watatu tangu kuidhinishwa kwake rasmi mwaka 2012.
1.Dk.Rajabu Mtumwa Lutengwe
2.Dk.Ibrahim Hamisi Msengi na
3.Jeneral Raphael Mugoya Muhuga wa sasa

Kwa ufupi kuhusu Mkuu Mkoa wa Katavi Raphael Mugoya Muhuga,huyu amewahi kuwa mkuu wa jeshi la kujenga taifa JKT mpaka alipostaafu utumishi wa jeshini 31 Januari mwaka 2016.
Kwa mjibu wa aliokuwa akiwaongoza,Katika kipindi cha uongozi wake ndani ya JKT, Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga alifanikiwa kuboresha kilimo, ufugaji, ujenzi wa miundombinu na malezi ya vijana wanaopatiwa mafunzo ya JKT.
Mikoa ya Rukwa,Katavi,Kigoma na Kagera wakuu wake wa mikoa ni waliowahi kuwa majenerali wa Polisi Tanzania ambapo baadhi ya wadau wa ulinzi na usalama wamesema kuwa huenda ikawa ni mpango mkakati wa serikali ya Tanzania Kupambana na uharifu unaotokea mipakani mwa nchi.
Mikoa ya Rukwa,Katavi na Kigoma inapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa Magharibi,Rwanda na Burundi Upande wa Kaskazini huku Mkoa wa Kagera ukipakana na Rwanda Upande wa Magharibi,Burundi upande wa Kusini na Nchi ya Uganda Upande wa Kaskazini.
ORODHA YA WAKUU WA MIKOA NA MIKOA WANAYOONGOZA
                          Paul Makonda                                        Dar es Salaam
                          Ezekiel Elias Kyunga                                  Geita
                          Salum Mustafa Kijuu(Jeshi)                        Kagera
                          Raphael Muhuga(Jeshi)                               Katavi
                          Emmanuel Maganga(Jeshi)                         Kigoma
                          Godfrey Zambi                                             Lindi
                          Dkt. Steven Kebwe                                       Morogoro
                          Zerote Steven(Jeshi)                                     Rukwa
                          Anna Malecela Kilango                                Shinyanga
                          Methew Mtigumwe                                       Singida
                          Antony Mataka                                              Simiyu
                          Aggrey Mwanri                                             Tabora
                          Martine Shigela                                             Tanga
                          Jordan Mungire Rugimbana                          Dodoma
                          Said Meck Sadick                                          Kilimanjaro
                         Magesa Mulongo                                            Mara
                         Amos Gabriel Makalla                                    Mbeya
                         John Vianey Mongella                                    Mwanza
                         Daudi Felix Ntibenda                                      Arusha
                         Amina Juma Masenza                                      Iringa
                         Joel Nkaya Bendera                                         Manyara
                         Halima Omary Dendegu                                  Mtwara
                         Dkt. Rehema Nchimbi                                     Njombe
                         Evarist Ndikilo                                                 Pwani
                         Said Thabit Mwambungu                                 Ruvuma
                       ChikuGalawa                                                Songwe(Mkoa mpya)


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA