KAMANDA KIDAVASHARI ATOA KAULI KUHUSU WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA UHARIFU MSIMU WA SIKUKUU YA PASAKA
Na.Issack Gerald-Katavi
JESHI la Polisi Mkoani Katavi limetoa onyo
kwa kikundi au mtu yeyote atakayesababisha vitendo vya furugu, fujo ama vitisho
vinavyosababisha uvunjifu wa amani katika kipindi chote cha kusheherekea
sikukuuu ya pasaka.
Kauli hiyo imetolewa
leo na kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ASP Dhahiri Kidavashari wakati akizungungumza
na vyombo vua habari kuhusu namna ambavyo jeshi la polisi limejipanga kuimarisha
usalama kipindi cha sikukuu pasaka.
Aidha, Kamanda
Kidavashari amewasisitiza wazazi/walezi kutowaachia watoto wao wadogo kuzurura
ovyo maeneo hatarishi kama vile barabarani,kuogelea kwenye madimbwi ya
maji/fukwe au kwenda maeneo ya mbali kutoka wanapoishi ili kuepusha kupotea au
kukumbwa na majanga yanayoweza kuepukika.
Wakati
huo huo,Kamanda Kidavashari anawaasa madereva wa vyombo vya moto kutokutumia
vileo kupita kiasi cha kushindwa
Comments