HABARI KUU 6 ZA WIKI ZILIZOTOKEZA KATAVI MACHI 21-27,2016 ,P5 TANZANIA MEDIA INAKUSOGEZEA
WAKAZI WAISHIO MLIMA WA LIAMBA LYAMFIPA WATAKIWA KUHAMA
KABLA NGUVU YA JESHI KUTUMIKA.
Na.Issack Gerald-Mlele
Baadhi
ya wakazi waliojenga nyumba na kuanza kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo
kilimo katika mlima wa Liamba Lyamfipa uliopo Wilayani Mlele Mkoani Katavi wametakiwa
kuhama mara moja sehemu hiyo.
Kupitia
kilele cha maadhimisho ya siku ya wiki ya maji yalifofikia kilele chake Machi
22 ambayo yalifanyika katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe,watendaji wa
vijiji,kata na wenyeviti wa vijiji wametakiwa kusimamia zoezi la kuwaondoa
wakazi hao.
Aidha
aliwataka wananchi kuwa waangarifu katika mlima huo na kutafakari madhara
yatakayojitokeza ikiwa mlima huo watauharibu.
Alisesema
wakazi watakaokaidi watafuatwa na mkuu wa Wilaya akiwa na Askari ili kuwatoa kwa nguvu.
Awali
katika ufunguzi wa maazimisho ya wiki ya maji duniani,serikali ya Mkoa wa
Katavi ilisema kuwa itaendelea kulinda vyanzo vya maji vilivyopo Mkoani Katavi
ikiwa ni sambamba na kutafuta namna ya kuendelea kutatua changamoto za baadhi
ya wananchi hususani kukosa maji.
Hata
hivyo baadhi ya wakazi katika Manispaa ya Mpanda walisema kuwa hawaoni haja ya
kuwa na maadhimisho ya wiki ya maji ikiwa mwananchi anaendelea kukosa maji ya
kunywa yaliyo safi na salama.
Maadhimisho
ya Wiki ya maji duniani huanza kila mwka machi 16 ha kufikia kilele chake machi
22.
C.W.T
YAWAMWAGIA MABATI WALIMU WASTAAFU MKOANI KATAVI
Na.Issack
Gerald-Mpanda
CHAMA
cha walimu C.W.T Mkoani Katavi kimekabidhi mabati 20 kwa walimu 11 wastaafu
kutoka katika halamshauri za Nsimbo na Mpanda kwa kila mmoja kama sehemu ya
kutambua mchango wao katika sekta ya elimu.
Akikabidhi
mabati hayo Machi 24,2016,mjumbe wa kamati ya C.W.T taifa Bw.Costantine Marisel
aliwataka walimu kuendelea kuzingatia maadili ya kazi yao.
Alisemakuwa
miongoni mwa tabia zinazotakiwa kuepukika ni pamoja na walimu wa kiume kutofanya
mapenzi na watoto wa kike,walimu wa kike kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike
na walimu kuwachangisha fedha wanafunzi fedha ambazo hazitakiwi kuchangwa kwa
kuwa kuna sera ya elimu bure.
Nao
baadhi ya walimu waliopata msaada huo walikishukuru chama cha walimu CWT kwa
kuwajali huku wakisema kuwa ni vizuri kuzingatia pia usafiri wao kutoka sehemu
moja kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao.
Hatua
hiyo pia ilipongezwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wazazi wakisema kuwa
hata taasisi nyingine zenye uwezo zifanye hivyo kwa ajili ya kuwasaidia kwa
kuwa walitoa mchango mkubwa katika utumishi wao.
HARAMBE YAFANYIKA MPANDA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MADAWATI,MAHITAJI
BADO LUKUKI
Na.Issack Gerald-Mpanda
Wadu mbalimbali wa elimu katika Manispaa
ya Mpanda na halmashauri ya Wilaya ya Mpanda wamefanya harambee na kupata kiasi
cha shilingi miloni 5 na elfu 65,madawati 224,mifuko 10 ya simenti na magogo 4
ya mbao kwea ajili ya kutengeneza madawati.
Machi 24,akizungumza wakati wa
harambee hiyo,mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bw.Pazza Tusamale
Mwamlia aliwapongeza wadau hao kwa michango hiyo na kuwaomba kuendelea
kuchangia kwa hiari.
Alisema kuwa Jamii haina budi
kuendelea kujitolea kuchangia madawati kwani kila suala haliwezi kukamilika kwa
kutegemea bajeti ya seriklai pekee.
Alisema kuwa changamoto ya madawati
kumetokana na ongezeko kubwa la wanafunzi waliojiandikisha darasa la kwanza
ambapo kwa kiwango cha juu baadhi ya shule zimesajili wanafunzi hadi 800 kwa
darasa la kwanza pekee.
Akisoma taarifa ya hali ya Mahitaji
ya madawati katibu wa wa kamati ya kuratibu na kutengeneza madawati Bw.Lukasi
Sotel Nyambala alisema kuwa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda ina upungufu wa
madawati 8245 ambapo imetengenza madawati 1500 huku yanayohitajika kutengezwa
yakiwa ni 7250 .
Kwa upande wa Manispaa ya Mpanda
Bw.Nyambala alisema kuwa ina upungufu wa madawati 5179 ambapo yaliyotengenezwa
ni 554 huku yanayohitajika kutengenezwa
yakiwa 4625.
Serikali ya Tanzania ilisema matarajio
ni ifikapo mwezi juni mwaka 2016 asiwepo mwanafunzi atakayekaa chini kwa
kisingizio cha kukosa dawati la kukalia.
WAHITIMU MAFUNZO
YA UHIFADHI HIFADHI ZA TAIFA WILAYANI KATAVI
Na.Agness Mnubi-Mlele
WAHITIMU
wa Mafunzo ya Kujengwa uwezo wa uongozi katika uhifadhi wa hifadhi za taifa
nchini wametakiwa Kujenga Mahusiano Mazuri na Jamii zinazozunguka hifadhi ili
kuwawezesha kupata taarifa za watu
wanaojihusisha na matukio ya ujangili.
Kauli
hiyo imetolewa na Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Katavi Luteni Kanali Alex Ntazi Wakati wa hafla ya Kufunga Mafunzo hayo iliyofanyika
Katika Kituo cha Mafunzo Kilichopo Wilayani Mlele Mkoani hapa.
Bw.Ntazi aliwataka wahitimu kuepuka vitendo
vya rushwa,matumizi mabaya ya silaha,ulevi na utovu wa nidhamu na badala yake
walinde rasilimali za taifa.
Aidha alisema wanatakiwa kuwa na
mahusiano na watu wanaozunguka maeneo ya hifadhi ili kupatiwa taarifa sahihi za
ujangili unaofanywa na waharibifu wa rasilimali za nchi.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mkuu
wa hifadhi za taifa Tanzania Bw.Ntango Mtaiko aliwataka wahitimu kuzingatia
nidhamu ya kazi na kupamana na ujangili na kudumisha ushirikiano kati yao
wenyewe na ndipo wahushe wengine.
Naye Mkurugenzi utumishi na utawala
hifadhi za taifa tanapa Bi.Witness Shoo aliwataka wahitimu kufauata
sheria,kanuni,taratibu na maelekezo katika kutekeleza majukumu.
Awali akisoma taarifa ya kituo cha
hifadhi cha mlele kaimu meneja mapori ya akiba Rukwa na Huhafwe Mark Chuwa
aliiomba idara ya wanyama pori hifadhi za taiafa na Mkoa wa kuujumla kutatua
changamoto zinazokikabili kituo hicho ikiwa ni pamoja na ufinuyu wa
bajeti,upungufu wa vitendea kazi,mawasiliano na miundombinu.
Katika risala ya wahitumu
iliyosomwa na mmoja wa wahitimu Bi
Angela Nyaki waliahidi kufanya kazi kwa weledi kwa kutumia mafunzo
waliyoyapata.
Mafunzo hayo ya wahifadhi
yaliyohitimishwa Machi 23,yaligawanyika katika makundi mawili amabpo kundi moja
lilianza Februari 01 mwaka huu na kumalizika Februari 16 mwaka huu huku kundi
la pili likianza Februari 22 na kuamlizika Machi 23 mwaka huu.
400
WABAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA KIFUAKIKUU KATAVI,IMANI ZA USHIRIKINA BADO
KIKWAZO.
Na.Issack Gerald-Nsimbo
Machi 24 kila mwaka ni maadhimisho ya
siku ya ugonjwa wa kifuakikuu duniani.Kupitia siku hiyo imegundulika kuwa Zaidi ya wagonjwa 400 wamegundulika kuwa na
maambukizi wa ugonjwa kipindupindu huku wagonjwa hao wakipatiwa matibabu na
habari njema ikiwa ni kuwa hakuna mtu aliyefariki kutokona na ugonjwa huo.
Takwimu hiyo iliotolewa na mratibu wa
kifuakikuu na ukoma Wilayani Nsimbo Mkoani Katavi Dk.Gabriel Kalumuna kwa niaba
ya Daktari wa kikufua kikuu Mkoa wa Katavi ambapo amesema kuwa kati ya idadi ya
wagonjwa hao hakuna kifo kichojitokeza na wote walipatiwa matibabu.
Alisema kuwa baadhi ya watu kuendelea
kuwa na imani za kishirikina zinachangia kuendelea kuwepo kwa ugonjwa huo kwani
watu huchelewa kupatiwa matibabu ambayo hata hakuna malipo yoyote.
Alisema kuwa vituo vinavyotoa huduma
ya kupima kifuakikuu katika Wilaya ya Mpanda ni Hospitali ya Wilaya ya Mpanda,Kituo
cha Afya Karema,Mwese na Mishamo huku vituo vyote vya afya vikitoa dawa kwa
wagonjwa.
Miongoni mwa vituo visivyokuwa na
uwezo wa kupima ni pamoja na Ilunde.
Aidha alisema kuwa idadi ya wagonjwa
ni wanazidi idadi ya vituo vya afya ambapo aliiomba serikali kuviwezesha vituo
vilivyoko mbali view na uwezo wa kupima wagonjwa hususani vijijini ambapo
vijiji vingi vipo Halmshauri za Wilaya ya Mlele ,Mpanda Vijiji,Mpimbwe na
Nsimbo.
Alisema kuwa ugonjwa huu husababishwa
na aina ya vimelea vijulikanavyo kama MICROBACTERIA CHUBA ambapo huenea kutoka kwa mtu mwenye maambukizi
kwenda kwa mtu mwingine asiye na maambukizi kupitia hewa.
Kuna aina mbili za kifuakikuu cha
mapafu ambazo hushambulia vioungo kama mifupa,figo,moyo na viungo vingine
mwilini ambapo kwa habari nzuri ugonjwa huu hutibika ikiwa mgonjwa atawahi
mapema kuanza matibabu.
Dalili za ugonjwa huu ni kukohoa kuanzia
mwezi mmoja na kuendelea,kukosa hamu ya chakula,homa za mara kwa mara makohozi yaliyochanganyika
na damu,kupungua uzito na kuhisi kifua kubanwa.
Njia moja wapo ya kupambana na ugonjwa huu ni
kujenga nyumba ambayo ina madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha na kuwahi
mapema katika vituo vya afya kupatiwa matibabu.
Kwa takwimu ya Wizara ya Afya,watu
wapatao 12000 hapa Tanzania hufariki dunia kutokana na ugonjwa huu.
RC
RAPHAEL MUHUGA AITAKA WILAYA YA MLELE KUTORUHUSU MAGARI KUPITA DARAJA LA MTO
KOGA
Na.Issack Gerald-Mlele
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral
Raphael Mugoya Muhuga aliuagiza uongozi wa serikali ya Wilaya ya Mlele
kutoruhusu magari kupita katika daraja la mto Koga unaotenganisha Mkoa wa
Katavi na Tabora.
Mkuu wa huyo wa Mkoa alitoa agizo
hilo Machi 25 alipokuwa amefanya ziara Wilayani Mlele.
Alisema kuwa magari madogo yasiyo ya
abiria ambayo yalikwishaanza kupita kutoka Mpanda Kuelekea Tabora yanaruhusiwa kupita
isipokuwa magari makubwa ya abiria yataruhusiwa kupita mpaka daraja hilo likatapofunguliwa
baada ya maji kupungua.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Mlele ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilayani humo
Bw.Issa Suleiman Njiku alisema kuwa mto huo hupokea maji kutoka mito ya Rungwa
na Chunya kupitia ziwa Rukwa huku akisema kuwa maisha yamepanda kwa wakazi wa
wilaya hiyo kutokana na usafiri kudhorota.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa
Halamshauri ya Wilaya ya Mlele Bw.Godwin Ben alisema kuwa tangu zuio liweke kwa
magari kupita eneo hilo hakuna gari lililokuwa likipita ambapo alisisitiza
kuwepo kwa usimamizi wa kutosha.
Mtalaamu wa wakala wa barabara
Tanroads kutoka makao makuu ya Mkoa wa Katavi alisema kuna haja ya kufanya ukaguzi
wa kina kuhakikisha usalama wa daraja unakuwepo muda wote.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa alitoa rai
kwa mkandarasi aliyepewa tenda ya kujenga daraja hilo kuanza matengenezo ya
daraja hilo haraka iwezekanavyo huku akisema kuwa kinachotakiwa ni kuangalia
namna ya kuongeza bidhaa mjini Inyonga kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu
waishio mlele.
Daraja la Mto Koga lilikatika Januari
26 mwaka 2016 na kupelekea vifo vya watu 10 baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kusombwa na maji.
Asante kwa kuchagua P5
TANZANIA MEDIA,ukiwa
na maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
na
endelea kufuatilia habari katika blog hii kwa kuandika P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments