WABUNGE VITI MAALUM MPANDA WATEMBELEA HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA,WATOA MSAADA WAAHIDI MAKUBWA.
Na.Meshack
Ngumba-Mpanda
SERIKALI
imeshauriwa kufanyia kazi changamoto zilizopo katika hospitali ya wilaya ya
Mpanda ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za afya.
Ushauri
huo umetolewa na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Bw. Naibu Mkongwa wakati
akizungumza na wabunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi Bi. Taska Mbogo na Bi. Anna
Lupembe walipotembelea hospitalini hapo.
Kwa
Upande wao wabunge hao wameahidi kushirikiana na uongozi wa hospitali, kwa kutoa
misaada itakayosaidia kupunguza kero ndogo ndogo kwa wagonjwa.
Katika
ziara hiyo pia wabunge hao wametembelea wodi mbalimbali za wagonjwa na kutoa misaada
mbalimbali ikiwemo sabuni za kufulia.
Katika
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda,kumekuwepochangamoto lukuki zikiwemo uhaba wa
dawa,hali tete ya usafi,wauguzi kutumia lugha isiyo na ustaarabu kwa wagonjwa
na uhaba wa vitanda hali inayosababisha wagonjwa wawili kulala kitanda komoja.
Comments