SILAHA 4 ZAKAMATWA KATAVI ZIPO MBILI ZA KIVITA WAMILIKI WAKE WATELEKEZA PIA PIKIPIKI WATOKOMEA KUSIKOJULIKANA WENYE GOBOLE WAO WADAKWA NA POLISI.
Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi la polisi Mkoani
Katavi,limekamata silaha nne zikiwemo silaha mbili za kivita aina ya SMG na
pikipiki moja aina ya Huoniao yenye namba za usajili T.948BHU za watu wanaosadikika kuwa ni majambazi.
Watuhumiwa waliokamtwa na silaha mbili aina ya gobole(PICHA NA.Issack Gerald Februari 26,2016) |
Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed akionesha miongoni mwa silaha ambazo zimekamatwa(PICHA NA.Issack Gerald Februari 26,2016) |
Katika picha ni Silaha aina ya SMG ambazo ni za kivita zikiwa ni miongoni mwa silaha 4 ambazo zimekamatwa (PICHA NA.Issack Gerald Februari 26,2016) |
Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi
ACP Rashid Mohamed amesema,silaha hizo aina ya SMG zenye namba AE 352720
na UA 3879 zenye risasi 62,zilkamatwa
jana Februari 25 majira ya saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha Kasekese Kata ya
Sibwesa Wilayani Mpanda zikiwa na magazine mbili.
ACP Mohamed alisema kuwa majambazi
hayo yalipokutana na askari wa doria yakiwa na pikipiki hiyo yenye rangi
nyekundi wakiwa na silaha hizo hawakutaka kusimama waliposimamishwa na Polisi
hao ambapo walitelekeza pikpiki na
hatimaye kutokomea kusikojulikana ambapo baada ya upekuzi kufanyika ndipo
zilipokutwa silaha hizo mbili za kivita aina ya SMG zikiwa na magazine mbili
zikiwa zimeviringishwa ndani ya suruali ya Jinsi na kufungwa kwenye tenga nyuma
ya pikipiki.
Wakati huo huo ACP Mohamed amewataja watu
wawili waliokamatwa Februari 24 majira ya usiku wakiwa na silaha aina ya Gobole
kuwa ni Donath Laurent(32) mkazi wa Nkungwi aliyekamatwa na silaha moja aina ya
gobole huku silaha hiyo ikiwa imefichwa kwa kuhifadhiwa kwenye majani nje ya
nyumba yake ambapo kwa upande wa Bw. Geofrey John Pandisha(34) mkazi wa Nkungwi
naye akikamatwa akiwa na silaha moja aina ya gobole akiwa nayo shambani kwa
ajili ya kuwinda wanyamapori ambapo wote ni wakazi wa kata ya Sibwesa Wilayani
Mpanda.
Watuhumiwa walikamatwa wanatarajia
kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika huku likiendelea
kuwasaka watuhumiwa wa ujambazi.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi
ametoa rai kwa wananchi wanaomiliki silaha ki nyume na utaratibu na kutaka
wasisalimishe silaha hizo mara moja ili kuepuka mkono wa sheria dhidi ya
wahusika wenye silaha kama hizo.
Comments