SERIKALI YATENGA SH. BILIONI 1.6 VYUO VYA UALIMU
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 1.65/- kwa
ajili ya mafunzo kwa vitendo kwenye vyuo vya walimu hapa nchini.
Alitoa
kauli hiyo jana (Jumamosi, Februari 27, 2016), wakati akizungumza na walimu na
watumishi wa sekta ya elimu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mtwara uliofanyika
kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara.
"Serikali
inatambua uhumimu wa mafunzo kwa vitendo katika vyuo vya ualimu ni kwa sababu
hiyo mwezi huu wa Februari tumetoa sh. bilioni 1.65/- kwa vyuo vya ualimu 35
vya umma nchini ili kuwezesha wakufunzi na walimu wanafunzi kushiriki
kikamilifu mafunzo kwa vitendo (Block Teaching Practice)," alisema huku
akishangiliwa.
Alisema
fedha hizo zinapaswa zitumike kulipia posho za kujikimu, nauli na ununuzi wa
vifaa vya kujifunzia na kufundishia.
Mapema, akizungumza na mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa, Waziri Mkuu alisema Serikali
imedhamiria kuimarisha elimu na akawaonya wote wanaowaharibia elimu watoto wa
kike.
"Tunataka
watoto wa kike wasome wa Kitanzania wasome hadi elimu ya juu waje wawe
watumishi wa umma hapo baadaye. Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake tukikumbuka
kaulimbiu ya Mama Salma Kikwete ya kwamba 'Mtoto wa Mwenzio ni wako',"
alisema.
"Yeyote
atakayemharibia mtoto wa kike masomo kwa kumrubuni na chips au pipi ajiandae
kwenda Lilungu, (gereza la mkoa wa Mtwara)", alisema.
Comments