MATUKIO YA WIKI KATAVI NA TANZANIA KWA UJUMLA FEBRUARI 8—13,2016.
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday,
February 09, 2016
Na. Agness Mnubi-Nsimbo
MAAFISA
tarafa,Watendaji wa kata na vijiji wa Halmashauri za Nsimbo,Mlele na Mpimbwe
wamepewa siku 4 za kutembelea shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika
Halmashauri zao ili kubaini upungufu wa madawati.
Agizo
hilo limetolewa jana na Mkuu wa Wilaya
ya Mlele Kanali Mstaafu Issa Suleiman Njiku katika kikao cha kamati ya ushauri
ya Wilaya ya Mlele kilichofanyika katika Halmashauri ya Nsimbo,na kuwataka
ifikapo February 12 kutoa taarifa za upungufu wa madawati.
Amesema
wanatakiwa kushirikiana ili kuzunguka katika shule za sekondari na msingi kufahamu idadi ya madawati yaliyopo na
pungufu .
Amesema
ifikapo february 28 Halamashauri hizo zinatakiwa kuwa zimetatua changamoto ya
upungufu wa madawati, huku Mkoa ukizitaka Halmashauri zote kutataua tatizo hilo
ifikapo mwishoni mwa mwezi machi mwaka
huu.
Halmashauri
zote nchini zinatakiwa kutekeleza agizo
la Serikali kuwa hakuna mwanafuzi anayetakiwa kukaa chini ifikapo juni 30.
UTAPELI
WA FEDHA ZA WALIMU KWA MTANDAO WAENDELEA KULINDIMA KATAVI,C.W.T KATAVI
YAWATAHADHARISHA WANACHAMA WAKE
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, February
10, 2016
Na.Issack
Gerald-Mpanda
Chama
cha walimu Tanzania (C.W.T) Mkoani Katavi,kimetoa tahadhari kwa wanachama wa
chama hicho na watumishi wengine kuwa makini kutokana na utapeli kwa kimtandao
ambao umejitokeza ukifanywa na watu wasiofahamika.
Tahadhari
hiyo imetolewa na leo na Mwenyekiti wa C.W.T Mkoani Katavi Mwalimu Gerigori
John Mshota wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio Fm
Ofisini kwake.
Amesema
kuwa kumezuka makundi ya watu wanaojitambulisha kuwa ni Viongozi wa C.W.T kikanda wakiwataka walimu wawape namba za
akaunti za benki ili walipwe mishahara yao.
Aidha
amesema kuwa Takribani watu wanne wakiwemo walimu walitapeliwa milioni kadhaa na watu wasiowafahamu kwa
kutumia mitandao ya mawasiliano.
Kati
ya walimu wawili ambao wamepokea mawasiliano kutoka kwa matapeli mwezi Februari
mwaka huu wakiwa katika harakati za kutapelewa yumo mmoja wa Shule ya Sekondari
Mwangaza iliyopo Manispaa ya Mpanda.
Amesema
kuwa amekuwa akijitambulisha kuwa yeye ni mlezi wa chama cha Walimu Tanzania
C.W.T katika mikoa ya Rukwa,Katavi na Kigoma.
Kwa
upande mwingine chama kimeliomba jeshi la polisi kusaidia kuwakamata watu
wanaojihusisha katika wizi wa kutumia mitandao.
Mwaka jana mbali na walimu kudai kutapeliwa
wengi wa wananchi walisema kuwa walitapeliwa fedha zao ambapo wimbi hilo
limeendelea kuwakumba waliowengi.
Katika
hatua nyingine mwenyekiti wa C.W.T amewataka walimu waliokuwa wakifanya kazi
kwa mkataba kutoka yaliyokuwa makazi ya wakimbizi na sasa makazi mapya,kuwa
wavumilivu wakati madai yao ya kupatindishwa madaraja na stahiki nyingine
zikiendelea kufanyiwa kazi na mamlaka husika.
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday,
February 09, 2016
Na.Issack
Gerald-Dodoma
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na
kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi
kiuchumi.
“Taarifa zilizopo zinaonyesha ni
asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo
inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi wanapata fursa
mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa
mchi yao,” alisema.
Waziri Mkuu amesema maeneo
yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na yanayogusa
maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi,
biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.
Ametoa kauli hiyo leo mchana wakati
akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano
cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo
2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa
na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia alizindua Mwongozo wa Utekelezaji
Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista Mhagama
alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye
halamhashauri zake na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.
Naye Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi, Prof. Omari Issa alisema katika dunia ya sasa imebainika kuwa haina
maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au kumuunganisha wadau wa
masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa kuwaunganisha na masoko.
OFISA
ELIMU AKANUSHA WANAFUNZI 21 KUTIMULIWA WAKITUHUMIWA KUVAA YEBOYEBO AMBAZO PIA
ZILICHOMWA MOTO.
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday,
February 10, 2016
Na.Issack
Gerald
WANAFUNZI wapatao 21 wanaosoma Shule
ya Msingi Kilambo cha Mkolechi, Kata ya Kala mwambao mwa Ziwa Tanganyika
wilayani Nkasi, wamefukuzwa shule kwa muda usiojulikana kwa kuvaa viatu maarufu
yeboyebo.
Imeelezwa kwamba yeboyebo hizo
zilikusanywa na kuchomwa kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kunatokana na waraka
uliotolewa na Ofisa Elimu Halmashauri ya Nkasi (Msingi) ukipiga marufuku
wanafunzi kuvaa aina hiyo ya viatu shuleni.
Hata hivyo,akizungumza kwa njia ya
simu akiwa mjini Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Ofisa Elimu Halmashauri
ya Wilaya ya Nkasi (Msingi), Misana Kwangula, alikanusha kutoa waraka huo kwa
shule hiyo.
“Sina taarifa rasmi ila (Jumatatu)
jioni alinipigia simu mkazi mmoja
akinitaarifu kwamba kuna mwalimu wa shule ya msingi Kilambo cha Mkolechi
amechoma moto viatu vya wanafunzi kwa madai kuwa ofisa elimu (msingi) ametoa
waraka kwamba wanafunzi hawatakiwi kuvaa yeboyebo shuleni…
“Hakuna waraka wala marufuku yoyote
iliyotolewa, isitoshe sio sahihi hata kidogo wala sio kitu kizuri kuchoma vifaa
walivyonavyo wanafunzi…. Sasa kama amewachomea wanafunzi hao viatu hivyo vya
yeboyebo basi awanunulie viatu vya ngozi,” alisema Kwangula.
Mkasa huo wa wanafunzi hao kufukuzwa
shule na kuchomewa yeboyebo walizovaa ulitokea juzi wakati wanafunzi hao walipofika
shuleni wakiwa wamevaa viatu hivyo. Inaelezwa kwamba mwalimu wa zamu, Baraka
Mwakasege aliwazuia kuingia darasani, badala yake akawaamuru wavue viatu vyao.
Taarifa kutoka shuleni hapo
zinaeleza kuwa, baada ya hatua hiyo, mwalimu huyo wa zamu alizikusanya yeboyebo
na kuzitia kiberiti kisha akawafukuza wanafunzi hao kwa muda usiojulikana hadi
wazazi na walezi watakapowanunulia viatu vya ngozi.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Posian
Ally alikanusha kumtuma mwalimu wa zamu kuwafukuza wanafunzi hao shule kwa muda
usiojulikana wala kuteketeza kwa moto yeboyebo zao. Alisema ataitisha kikao ili
kujadili suala hilo na kwamba mwalimu huyo akibainika kutenda kosa hilo
ataamriwa kuwanunulia watoto hao viatu vingine.
Akizungumza mmoja wa wazazi wa
wanafunzi hao, Privatus Yoram, alithibitisha kutokea kwa mkasa huo. “Jana jioni
nilimwona mwanangu anayesoma darasa la tano shuleni hapo akirudi nyumbani akiwa
peku.
Nikamuuliza kulikoni, akanieleza
kuwa mwalimu wa zamu (Mwakasege) amewafukuza shule na kuchoma yeboyebo zao kutokana
na waraka wa Ofisa Elimu Nkasi unaopiga marufuku yeboyebo shuleni,” alisema
Yoram.
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday,
February 11, 2016
Na.Issack
Gerald-Mpanda
Bweni
la wavulana la Shule ya Sekondari ya Sanny inayomilikiwa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) limeteketekea kwa moto na kuteketeza mali zote za
wanafunzi.
Mkuu
wa Shule ya Sanny Sisiter Anna Usiri amesema kuwa tukio hilo ambalo limetokea
leo majira ya saa 12 Alfajiri hakuna mwanafunzi aliyepatwa madhara kiafya mbali na mali zao zote kuteketea.
Aidha,Mkuu
huyo wa shule,ametoa hofu wazazi wa wanafunzi hao kuwa hawatakosa mahali pa kulala licha ya bweni lao kuungua
ambapo pia wataendelea na masomo kama kawaida.
Amesema
kuwa katika bweni hilo,vitu ambavyo vimetketea ni magodoro,sare za shule,baadhi
ya daftari na vitabu.
Kwa
upande wake kiongozi wa bweni hilo ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha pili
katika shule hiyo Bw. Ansel Felisian amesema kuwa waliamka alfajiri ya saa 12
na kwenda darasani kusoma ambapo tukio hilo lilijulikana baada ya mwanafunzi wa
kidato cha kwanza kutoa taarifa kwa kiranja huyo baada ya mlinzi wa shule
kumwagiza akatoe taarifa juu ya hali hiyo.
Kwa
upande wake Kamanda wa jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoani Katavi Mrakibu Nestory Kisenya Konongo amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema wamesaidia kuzima moto huo baada ya
kupata taarifa za tukio hilo.
Shule
hiyo ina wanafunzi 31 waliokuwa wakiishi katika bweni hilo huku shule hiyo
change yenye kidato cha kwanza hadi cha tatu ikiwa na jumla ya wanafunzi 66
pekee.
Hata hivyo chanzo cha ajali hiyo ya
moto hakijafahamika na uchunguzi unaendelea kufanyika
RIPOTI YA PILI AJALI MTO KOGA : MIILI
YA WATU WALIOKUFA MAJI MTO KOGA HADI SASA HAWAJAPATIKANA NA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA.
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday,
February 11, 2016
Na.Issack
Gerald-Katavi
Miili
5 ya watu waliozama katika mto Koga uliopo mpakani mwa Mkoa wa Tabora na Katavi
baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji tarehe Januari 26 ,2016
hawajapatikana pamoja na gari walilokuwa wakisafiria.
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoani Katavi ambaye
pia ndiye Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk.Ibrahim Hamis Msengi wakati akizungumza na
P5 TANZANIA MEDIA Ofisini kwake.
Dk
Msengi amesema kuwa mpaka sasa hakuna gari linaloweza kupita kutokana na maji
yanayozidi kuongezeka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na maji kujaa kwa
wingi.
Katika
hatua nyingine Dk Msengi amesema kuwa ukarabati wa barabara ya kutoka Mpanda
hadi Tabora unaendelea kufanyika kwa kiwango cha lami isipokuwa eneo lilipo
daraja la mto Koga ndipo bado kuna utata kutkana na wingi wa maji hayo.
Hata
hivyo katika hali ya ukiukwaji wa onyo linalotolewa na viongozi,kuna watu
wanaoendelea kusombwa na maji hayo kutokana na kudharau katazo hususabi
wanaotoka Tabora kuja mpanda.
HABARI
YA ASKARI WA KIKE WA USALAMA BARABARANI KUTEKETEA KWA MOTO NA MPENZI WAKE
MKOANI RUKWA HII HAPA,PIA UTAJUA KILICHOTOKEA KWA WATOTO WAWILI WADOGO
WALIKUWEMO
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, February
12, 2016
Na.Issack
Gerald-Rukwa
ASKARI
wa kike wa Usalama Barabarani, Attuganile Mwakibete (37) na mpenzi wake Sunday
Mhagama (36), wameteketea kwa moto baada ya nyumba walimokuwa ndani kuungua.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda amesema tukio hilo lilitokea Februari
2, mwaka huu saa 7:15 mchana katika kitongoji cha Maporomoko, Kata na Tarafa ya
Laela Wilaya ya Kipolisi ya Laela.
Inadaiwa
kuwa nyumba hiyo iliyoteketea kwa moto ambayo askari Attuganile alikuwa
amepanga vyumba viwili, ni mali Yaiyela Mwamahonje aliyokuwa akiishi na watoto
wake wawili wadogo ambao wamenusurika kufa, licha ya kuwemo ndani ya nyumba
hiyo wakati wa ajali hiyo.
Taarifa
za uhakika zinaeleza kuwa Mhagama aliyekuwa rafiki wa trafiki huyo wa kike, ni
mkazi wa Mbeya ambako mkewe anaishi, na alikuwa na mazoea ya kumtembelea mpenzi
wake huyo mara kwa mara.
Inadaiwa
askari Attuganile alikuwa ameachana na mumewe wa ndoa. “Vyumba viwili yaani
sebule na chumba walimokuwemo Attuganile na Mhagama viliwaka moto baada ya
jenereta lililokuwa likifanya kazi likiwa sebuleni humo kulipuka na kuwajeruhi
vibaya,” alieleza.
Kwa
mujibu wa Kamanda Mwaruanda,Attuganile alifariki dunia Februari 8, mwaka huu
saa 2:30 asubuhi akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini
Sumbawanga.
Mhagama
alikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya jijini Mbeya
ambako alifariki dunia Februari 9, mwaka huu ambapo hata hivyo kamanda
Mwaruanda alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Chanzo:Jeshi la Polisi Rukwa,endelea kufuatilia P5 TANZANIA
MEDIA
MTANDAO
WA RADIO ZA JAMII (COMNETA) WAZUNGUMZIA SIKU YA RADIO DUNIANI INAYOFANYIKA FEBRUARI
13,KILA MWAKA.
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, February
12, 2016
Na.Issack
Gerald-Katavi
Mtandao
wa Radio za Jamii Tanzania (COMNETA) umetoa rai kwa viongozi wa ngazi
mbalimbali kuanzia ngazi ya seriklai za mitaa mpaka ngazi ya taifa,kutumia
radio mara kwa mara kwa lengo la kuelimisha na kufikisha ujumbe katika jamii
kuliko kiongozi kutumia radio kwa wakati Fulani kwa maslahi binafsi.
Rai
hiyo imetolewa leo na viongozi wa mtandao huo Tanzania na umoja wa
Mataifa,wakati wa mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC kuhusu siku
ya radio duniani ambayo inatarajia kuadhimishwa kesho duniani kote.
Katika
mahojiano hayo, Mwenyekiti wa Mtandao huo Bw.Joseph Sekiku amesema kuwa redio
za jamii Tanzania zimesaidia katika utatuzi wa migogoro baina ya wakulima na
wafugaji kwa kuelimisha jamii matumizi
bora ya ardhi pamoja na kuunganisha watawala na watawaliwa kwa lengo la
kudumisha amani na kutatu migogoro hiyo kwa mazungumzo.
Amewaasa
viongozi wa umma katumia vyombo mbalimbali vya habari za kijamii kufikisha
ujumbe kwa kuwa radio zipo kwa ajili kuelimisha,kuburudisha,kuasa na
kuhabarisha.
Kwa
upande wake Meneja wa Mpanda Radio Fm ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa mtandao wa Radio za jamii (COMNETA) Bw.Prosper Laurent Kwigize amesema kuwa vyuo mbalimbali
vinavyoendesha mafunzo ya uandishi,utangazaji na taaluma yote ya habari kwa
ujumla,vinatakiwa kuwa na wakufunzi wenye weledi wa taaluma ya habari ili kupata watalaamu wa taaluma hiyo wenye
uwezo wa kusaidia jamii na kuepuka kuendelea kuwa wanafunzi wanapopata kazi
katika taasisi.
Aidha
Bw.Prosper amesema kuwa wanasiasa wanatakiwa kutambua umuhimu wa radio hata
baada ya kampeni za uchaguzi kufanyika kuliko kutambua vyombo vya habari wakati
wa kampeni za kusaka kura pekee na baada ya hapo kutorejea kuzungumza na
waliompigia kura ili watambue ni kitu gani kinachoendelea katika kushughulikia
ahadi zake.
Katika
mahojiano hayo,Bi.Stela Vuzo ambaye ni Afisa Habari kutoka umoja wa Mataifa
aliyeko hapa nchini mbali na kuvitaka vyombo vya habari kufuata miongozo ya
vyomvo vya habari kuepuka uvunjifu wa amani nchini.
Wakati
huo huo,amewataka wanawake na vijana kutumia vyombo vya habari ikiwemo radio
kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili na masuala ya kijasiliamali.
Kwa
mjibu wa Shirika la kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limesema
kuwa jumla ya watu milioni 20 duniani Kote wanasikiliza na kutegemea radio
katika kuzungumzia masuala mbalimbali ya kijamii.
Maadhimisho
ya siku ya Radio Duniani huadhimishwa ila mwaka ifikapo Februari 13,ambapo kwa
mara ya kwanza maadhimisho haya yalifanyika mwaka 1946 kote duniani.
Kauli mbiu ya siku ya Radio Duniani “REDIO KAMA CHOMBO CHA HABARI
WAKATI WA MAJANGA”.
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, February
12, 2016
Na.Issack Gerald
SERIKALI imeamua kuwasimamisha kazi
watendaji wawili kutoka Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuanzia leo ili kupisha
uchunguzi wa upotevu wa mafuta bandarini kutokana na zuio la kufunga kwa mita
kwa zaidi ya miaka mitano.
Waliosimamishwa kazi ni Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa na Meneja Vipimo
Kitengo cha Bandari, Bi. Bernadina Mwijarubi. Bi. Mwijarubi ndiye
anashughulikia kitengo cha mafuta bandarini.
Akitangaza uamuzi huo kwenye kikao
cha Makatibu Wakuu kilichofanyika leo Februari 12, 2016) ofisini kwake Magogoni
jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Mkuu wa
Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Adelhelm Meru awaandikie barua za
kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi huo.
“Katibu Mkuu Viwanda,
waandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi. Katika kipindi
hiki hawatatakiwa kusafiri kwenda popote hadi uchunguzi utakapokamilika. Pia
utafute mtu wa kukaimu nafasi hiyo ili kazi ziendelee,” alisema.
Waziri Mkuu pia amesema ofisi
yake itawaandikia barua ofisi ya TAKUKURU na polisi ili wafuatilie suala hilo
mara moja na ikithibitika kuwa walihusika hatua rasmi zitachukuliwa na
itathibitika hawakuhusika basi watarudishwa.
Waziri Mkuu pia aliagiza mfumo wa
upimaji mafuta kwa kutumia flow meters uendelee kutumika na ule upimaji
wa kukadiria uache kutumiwa mara moja.
Jana (Alhamisi, Februari 11, 2016)
Waziri Mkuu alifanya ziara kukagua flow meters za zamani zilizopo
Kurasini (Kurasini Oil Jetty) na kisha akatembelea na kukagua flow meters
mpya ambazo zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu dola za marekani milioni
6 (sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).
Pia Waziri Mkuu alitembelea sehemu
ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na
kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya
TIPER yaliyoko Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia baina ya Serikali na kampuni
ya Oryx Energies.
Katika ziara hiyo ilibainika kuwa
Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba
kubwa la mafuta linalotoka bandarini hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza
kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.
“Jana niliagiza kuwa bomba hilo
ling’olewe. Nimetoa mwezi mmoja ili kurekebisha mfumo huo. Simamieni vizuri na
kuhakikisha kuwa na wao pia wanarudi kwenye manfold kama ilivyo
kwa wengine,” alisema Waziri Mkuu.
Saturday, 13 February 2016
IDARA YA ELIMU YATOA TAARIFA RASMI MFUMO MPYA WA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI KUFANYA MITHANI MWAKA 2016 MPANDA,SHULE ZISIZOSAJILIWA NJIAPANDA
Posted By:Issack
Gerald | At:Saturday, February 13, 2016
Na.Issack Gerald-Mpanda
Idara ya elimu Shule za Msingi katika
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imewataka wazazi na walezi wa watoto wanaosoma
katika shule ambazo hazijasajiliwa mkoani katavi ikisema kuwa kuna uwezekano wa
wa kupoteza pesa nyingi na wanafunzi kukosa nafasi ya kufanya mitihani
mbalimbali ya shule ya msingi inayotambuliwa na Wizara ya
elimu,Sayansi,Teknolojia na ufundi.
Rai hiyo imetolewa jana na Afisa
elimu Taaluma Elimu ya msingi Manispaa ya Mpanda Bw.Rashid Pili katika taarifa
yake ambayo ameitoa kwa vyombo vya habari.
Amesema kuwa huenda wanafunzi wengi
wakakosa kufanya mtihani yao kutokana na wengi wa wanafunzi kujiunga na shule
ambazo hazijasajiliwa katika Manispaa ya Mpanda na hata Mkoa wa Katavi kwa
ujumla.
Aidha Bw.Pili amesema kuwa mfumo mpya
wa kufanya mitihani unaoanza mwaka 2016 unahusisha wanafunzi wa darasa la
pili,la nne na la saba ambapo mithani hiyo itasimamiwa na balaza la mtihani la
taifa(NECTA).
Hata hivyo wazazi wameshauliwa
kuwahamisha watoto wao katika shule ambazo hazijasajiliwa na kuwapeleka katika
shule za serikali zilizosajiliwa au zile za binafisi.
Kwa mjibu wa taarifa hiyo,katika
Manispaa ya Mpanda kuna shule 34 za serikali zitakazokuwa na vituo vya kufanyia
mtihani huku shule 2 pekee zinazofundisha Kiingereza za Reimeta English Medium
School na Nzera English Medium Schoolsnazo pia zikiwa zimesajiliwa wanafunzi
wake kufanya mtihani.
Katika hatua nyingine,Bw.Pili amesema
kuwa usajili wa wanafunzi watakaofanya mtihani ngazi ya shule ulikwishakamilika
mwaka huu ambapo usajili unaoendelea kwa sasa ni kwa ngazi ya Halmashauri
wakati huo huo mchakato wa kuyaingiza majina ya wanafunzi hao katika mtandao wa
balaza la Mtihani NECTA ukiendelea.
Miongoni mwa shule ambazo
hazijasajiliwa kwa mjibu wa Afisa elimu huyo ni pamoja na shule ya msingi
Motherland ambapo mpaka sasa ina wanafunzi wanaosomea katika shule hiyo.
Usikose kitachozungumzwa na shule zenye wanafunzi zikisemekana
kutsajiliwa na wanafunzi kutofanya mitihani,endelea kuwa na P5 TANZANIA
MEDIA na Mpanda Radio Fm
Comments