KIKAO CHA WATALAAMU,WATENDAJI NA WAKUU WA IDARA MBALIMBALI MANISPAA YA MPANDA KUFANYIKA KESHO.
Na.Issack Gerald-Mpanda
Kikao cha kujadili masuala mbalimbali
ya maendeleo katika Manispaa ya Mpanda kinatarajia kufanyika kesho.
Kwa mjibu wa taarifa ya Afisa habari
wa Manispaa ya Mpanda kwa vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi Manispaa ya
Mpanda,Bw.Pius Donald amesema kuwa,kikao hicho kinatarajia kufanyika katika
ukumbi wa idara ya maji kuanzia majira ya Asubuhi.
Kikao hicho kitakachowashirikisha
waandishi wa habari,pia kinatarajia kuwahusisha watalaamu mbalimbali wakiwemo Mkurugenzi
wa Manispaa ya Mpanda,wakuu na watendaji wa idara mbalimbali katika Manispaa ya
Mpanda.
Kikao hiki kinafanyika ikiwa ni siku
chache baada ya vikao vya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017
kufanyika karibu Halmashauri zote tano za Mkoa wa Katavi.
Comments