JIPU KUBWA MPANDA KATAVI LATUMBULIWA,WATUMISHI 16 NJE,TUME KUANZA KAZI YAKE WATAKAOBAINIKA SHERIA ZANOLEWA YUMO NA MWANASHERIA WA MANISPAA YA MPANDA.
Na.Issack Gerald-Mpanda
BALAZA la
Madiwani Katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ,limewasimamisha kazi watumishi 16 wa Manispaa hiyo
kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo utumiaji ovyo wa fedha za manunuzi ya gari la kuzoa
taka pamoja na ubadhilifu wa fedha ya skimu ya umwagiliaji maji ya kakese.
Watumishi hao 16,wamesimamishwa kazi
kupitia kikao cha dharula ambacho kimefanyika jana Februari 26 katika ukumbi wa
Manispaa ya Mpanda.
Akitangaza majina ya waliosimamishwa
kazi,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Philip Mbogo,amewataja kuwa
ni Bw.Chamilius Luhinda mwanasheria wa
Manispaa,Vumilia Kakulima mkuu wa kitengo cha Manunuzi,Charles Ngonyani mkuu wa
idara ya ushirika,chakula na umwagiliaji,Brian Severe mkuu wa idara ya ardhi
mipango miji na maliasili,Vicent Kayombo mkuu wa idara ya elimu Shule ya
Msingi,Abrahamu Kaswa afisa mipango miji,Bosko Kapinga mweka hazina wa
Manispaa,Kibi Hamis Musaka Mhasibu Mwandamizi,Paschal Kweya afisa afya Mazingira
Manispaa ya Mpanda,Gerigori Lugarema afisa maendeleo ya jamii msaidizi,Gorge
Ngongolowo mhasibu mwandamizi,Albert Kiando mhandisi wa ujenzi,Victa Lutajumula
mwalimu Mkuu daraja la pili,Focus Bilamule mhasibu Manispaa ya Mpanda,Jefu Julious mhandisi umwagiliaji Manispaa na Said Madua
Afisa mazingira wa Manispaa ya Mpanda.
Mh.Mbogo amewataja wanaokaimu nafasi
hizo kuwa ni pamoja na Said Mohamed Hemed mkuu wa idara ya ushirika,chakula na
umwagiliaji,Rashid Pili Idara ya elimu Msingi,Mabokera Mwakabamba kitengo cha
Manunuzi,Paschal Sindani idara ya ujenzi,Juma Luhomwa mweka hazina wa Manispaa
huku Peter Charles Mkalipa atakaimu mkuu
wa idara,ardhi na maliasili.
Hata hivyo Mh.Mbogo amesema kuwa
nafasi ambazo hawajapatikana watakaokaimu nafasi zao kwa sasa utaratibu
unaendelea ili kutokwamisha shghuli za Manispaa.
Kutokana na kusimamishwa kwa
watumishi hao,balaza la madiwani limetaka kuundwa tume ya kuchunguza tuhuma
hizo kwa ajili ya kuchulia hatua zaidi kwa wale watakaokuwa wamebainika zaidi.
Mwezi uliopita,Mkurugenzi Mtendaji
Manispaa ya Mpanda Bw.Suleimani Lukanga alismamishwa kazi kwa tuhuma za
kuhusika katika mamununuzi hewa ya gari ta kuzoa taka na kutapanya pesa za umwagiliaji ambazo
zilikuwa zaidi ya milioni 380 ambapo alisimamishwa na Waziri wa Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa TAMISEMI.
Endelea kuwa na P5 TANZANIA MEDIA.
Comments