AGIZO LA WAZIRI KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA WAKULIMA WA TUMBAKU KATAVI BADO NDOTO,MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA KATAVI ATOA UFAFANUZI.
Na.Issack Gerald-Katavi
Agizo la naibu waziri wa
kilimo,mifugo na uvuvi Mh.Willium Tate
Ole Nashe la kumtaka mrajisi vya vyama vya
ushirika hapa nchini kuteua timu
ya kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku wa Chama cha Ushirika
Mpanda Kati wanaolalamika kutolipwa madai yao karibu milio 600
halijatekelezwa.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na
Mpanda Radio fm Ofisini kwake,Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Katavi
Bw.Luhiguza Medadi Sesemukwa amesema kuwa,taarifa iliyopo kutoka kwa
mrajisi ngazi ya taifa aliyeagizwa
kufanya ukaguzi huo amesema timu hiyo
imechelewa kufika kutekeleza agizo la waziri kutokana na ukosefu wa fedha.
Bw.Sesemukwa amesema kuwa,wajumbe wa
timu kutoka tume ya maendeleo ya ushirika
iliyoundwa na mrajisi wa vyama vya ushirika nchini inatarajia kufika
Mkoani Katavi wakati wowote kuanzia leo.
Hata hivyo shirika la wakaguzi wa
vyama vya ushirika COWASCO kutoka Mkoani Tabora kwa sasa wapo Mkoani Katavi kuanzia
Februari 14 mwaka huu na wanaendelea ukaguzi wa madai ya wakulima.
Amesema mara baada ya timu kutoka
Dodoma ambako ndiko makao makuu yao yaliko,wataungana na timu timu iliyotoka
Tabora kwa ajili ya kuendelea na ukaguzi na uchunguzi wa kina.
Agizo la naibu waziri wa
kilimo,mifugo na uvuvi Mh.Willium Tate
Ole Nashe la kumtaka mrajisi vya vyama vya
ushirika hapa nchini kuteua timu
ya kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku wa Chama cha Ushirika
Mpanda Katavi wanaolalamika kupokonywa mamilioni hayo ya fedha,lilitolewa
Januari 11,mwaka huu akitoka agizo la kuundwa na kutumwa timu ya ukaguzi ndani
ya siku 14 kuanzia siku ya agizo kutolewa.
Katika hatua nyingine amewataka wakulima
waliotoa hoja ya madai yao kutuo uthibitisho wa vielelezo ili kubaini ukweli wa
malalamiko.
Mbali na malalamiko ya kutoripwa
kitita hicho karibu miloni 600,pia walilalamikia kulipwa kwa thamani ya dola badala ya
shilingi,kuuziwa pembejeo kwa bei kubwa na kulipa kwa dola na kutokuona msaada
wa Chama kikuu cha ushirika LATCU kwa wakulima wa zao la tumabku badal aya
kuwanyonya.
Wakati huo huo,amewashauri Mrajisi
Sesemukwa ametoa rai kwa wakulima kuendelea kupanda miti,kutumia Mabani ya
kisasa ya kuchomea tumbaku yanayotumia kuni kidogo kwa ajili ya kuhifadhi
mazingira.
Lakini pia amewataka wakulima
kutotorosha tumbaku na kwenda kuuzia nje ya kampuni iliyoidhinishwa kununua
tumbaku yake ili kuepuka kusababisha mlundikano wa madeni watakayodaiwa.
Majibu ya mrajisi wa Mkoa,yanakuja
kufuatia malalamiko ya wakulima kuanza kujitokeza wakilalamika kutokuona agizo
la waziri kutotekelezeka.
Comments