BREAKING NEWS : WAZIRI MKUU LEO KUANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI RUVUMA
NA:OFISI YA WAZIRI MKUU
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku nne
mkoani Ruvuma, ambapo atawasili mkoani hapo leo saa tisa alasiri.
Waziri Mkuu wa TANZANIA Kassim Majaliwa (PICHA na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Baada
ya Waziri Mkuu kuwasili Uwanja wa Ndege wa Songea, atapokelewa na viongozi wa
Chama na Serikali, pia atakwenda Ikulu kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa
Ruvuma.
Aidha,
siku ya jumatatu atakuwa na shughuli za kufungua tawi la Benki ya
Posta mjini Songea, kukagua maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi
ya chakula (NFRA) kanda ya Songea na kukagua makao makuu ya
Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Siku
inafuata atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya mkoa, na baadaye
kuzungumza na watumishi wa hospitali hiyo.
Siku
ya nne ya ziara yaani jumatano, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara mkoani
humo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea Dar es
Salaam.
Nifuatilie zaidi kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM kuhusu kitakachokuwa kikiendelea mwanzo hadi mwisho wa ziara ya Waziri Mkuu
Comments