WAZIRI MKUU AHITIMISHA ZIARA YA SIKU MBILI KIGOMA ATAJA MKAKATI WA SERIKLAI KUPANUA BANDARI ZIWANI TANGANYIKA
Na.Issack Gerald-KIGOMA
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Halimashauri ya Manispa Kigoma Ujiji
kwa kubuni miradi mbalimbali ya biashara katika ziwa Tanganyika na tekinolojia mpya ya kukausha dagaa
wanaovuliwa katika ziwa hilo.
Amebainisha hayo alipokuwa
akizungumza na wananchi pamoja na
wafanya biashara wa kata ya kibilizi mkoani kigoma alipoanzia ziara yake mkoani
humo.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua dagaa wanaokaushwa kitalaam kwa kutumia jua wakati alipozindua soko na mwaro wa kisasa wa samaki wa Kibirizi mjini Kigom. Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) |
Pamoja na hayo waziri mkuu amesema
serikali ipo kwenye mkakati wa kupanua
bandari ya ziwa Tanganyika ili dagaa na samaki wanaovuliwa humo waweze kupata soko na
kusfiriishwa katika nchi jilani za Congo,Burundi na nchi nyingine
Hata hivyo waziri mkuu Kasm Majaliwa amesema kuwa atahakikisha
suala la usalama unaimarishwa kwani
wavivu wa ziwa hilo walikuwa wakifanya kazi zao za uvuvi katika mazingira sio salama.
Wakati huo huo Waziri Mkuu jana amehitimisha
ziara yake ya siku mbili mchana na kurejea Jijini Dar es Salaam.
Comments