WAZAZI WATAKIWA KUHAKIKISHA WAANDIKISHA DARASA LA KWANZA WATOTO WAO
Na.Issack Gerald-MPANDA
SERIKALI Imewataka Wazazi wote
Kuhakikisha Watoto waliofikia Umri wa Kuanza Shule Kuandikishwa na Kuahidi
kuwachukulia hatua watakaoshindwa Kutekeleza agizo hilo.
Zoezi la Kuandikisha Wanafunzi wa
Darasa la Kwanza na awali limeanza leo Katika shule mbalimbali nchini na
litadumu kwa Kipindi cha Mwezi mmoja.
Kituo hiki Kimezungumza na Bw.Lazaro Njau Mwalimu Mkuu Katika Shule ya
Msingi Mpanda ili Kufahamu idadi ya Wanafunzi wanaokusudiwa Kuandikishwa Katika
shule hiyo.
Shule ya Msingi Mpanda yenye jumla ya
wanafunzi 1,492 imeweka Malengo ya Kuandikisha wanafunzi 186 wa Darasa la
Kwanza na 136 wa Darasa la awali.
Comments