WATATU KATAVI WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI
Na.Issack
Gerald-Mpanda
Jeshi la polisi Mkoani Katavi linawashikilia
watu watatu kutokana na kukamatwa na nyara za serikali ambazo wamezipata
kinyume na sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri
Kidavashari amewataja wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Leonard Mbegele(38)
mkazi wa Migazini na Anastazia Bernad(38) mkazi wa kichangani ambao walikamatwa
mnamo tarehe 22.12.2015 majira ya saa 13:00 maeneo ya Mikocheni Tarafa ya
Kashaulili Wilayani Mkoani Katavi wakiwa na nyama ya Kongoni kilo moja.
Kamanda amesema kuwa Jeshi la Polisi baada
ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema lilifanya upekuzi nyumbani kwa Anastazia
Bernard ambapo nyama hiyo ilikutwa ikiwa imewekwa kwenye Hotpot iliyokuwa ndani
ya kabati.
Katika upelelezi wa awali wa tukio hiliAanastazia
alidai kuwa nyama hiyo ni ya Malack Jonas ambapo hata hivyo Jonas naye aliikana
nyama hiyo.
Mpaka sasa watuhumiwa wote wanashikiliwa kwa
mahojiano zaidi na watafikishwa mahakamani baada ya Upelelezi kukamilika.
Wakati huo huo Leornard Mbegele (38) Mkazi
wa migazini Kata ya Nsemulwa, Tarafa ya Kashaulili, Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi
Mnamo tarehe 22.12.2015 majira ya saa 14:00 anashikiliwa na alikamatwa akiwa na nyama ya
Kongoni kilo 15.
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishewa mahakamani
upelelezi utakapokamilika.
Comments