WANAWAKE MPANDA NDOGO NA KABUNGU WAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI
Na.Issack Gerald-MPANDA
Jumla ya watu 14 kati ya 169
waliopima Virusi vya Ukimwi Mwezi Novemba mwaka huu katika Kata ya Kabungu na
Mpanda Ndogo wamegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Hayo yamebainishwa na Bahati Mwailafu Afisa ustawi wa Jamii ambaye
pia ni Kaimu Mratibu wa Ukimwi Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda,wakati
akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA
Ofisini kwake kuhusu mikakati ya Halmashauri kupamba na Ugonjwa wa Ukimwi.
Aidha Mwawilafu amesema kuwa Halmshauri
itaendelea kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika
kata zote 16 za Halmashauri hiyo.
Katika takwimu za maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi ambazo zimeapatikana kwa kipindi cha mwezi Novemba mwaka huu
toafauti na takwimu ambayo imekuwepo katika kata mbili kati ya 16 inaonesha
kuwa kata ya Kabungu jumla ya waliopima
virusi vya Ukimwi ni 117,Walioatharika-8
kati yao Wanawake-6 na Wanaume-2 huku Kata
ya Mpanda ndogo Walioapima wako 52,Wanawake-43 na Wanaume-09 ambapo wathirika ni mwanaume 1 na wanawake -5
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiraia ya UDESO Eden
Ezekiel taasisi ambayo makao makuu yako Usevya katika Wilaya ya Mlele ametoa
shukrani kwa wafadhiri mbalimbali wakiwemo watu wa Marekani wanaochangia nguvu
kubwa kupambana na virusi vya Ukimwi na kuishauri serikali kuwekeza bajeti
kubwa katika mapambano ya Ukimwi .
Hata hivyo wakazi wote Mkoani Katavi wametakiwa
kutumia elimu wanayopewa kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mkoa wa Katavi una asilimia 5.9 ya
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika utafiti uliofanyika miaka ya hivi
karibuni.
Siku ya Ukimwi duniani huadhimishwa
Desemba Mosi ya Kila mwaka.
Comments