WAKAZI MPANDA WACHARUKA KUANDIKIWA RISITI TOFAUTI NA PESA WANAYOLIPA KWA USHURU WA KUZOA TAKA
Na.Issack
Gerald-MPANDA
BAADHI ya wakazi wa
mtaa wa Mpanda Hotel C Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamelalamikia
hatua ya kupewa lisiti iliyoandikwa fedha tofauti na kiasi wanacholipa kwa ajili
ya kuzoa taka katika mtaa huo.
Wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA wamesema wamekuwa
wakipewa lisiti zilizoandikwa shilingi mia tano badala ya shilingi elfu moja
wanayolipa kama utaratibu wa Manispaa unavyoelekeza.
Wakazi hao wameitaka Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda kuweka
nafasi ya kuandika jina la mchangiaji wa mchango wa ushuru katika lisiti
tofauti na ilivyo sasa ambapo listi hiyo haioneshi jina la mchangiaji.
Hata hivyo mjumbe wa
mtaa wa Mpanda Hotel C Leonard Sokoni aliyehusika
kutoa lisiti hizo, amekiri kukiuka utaratibu wa utoaji lisiti hizo na ameahidi
kurudia kutoa lisiti nyingine kama utaratibu unavyoelekeza.
Comments