TANROAD KATAVI WATAJA MIKAKATI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATAVI

Na.Issack Gerald-MPANDA 
WAKALA wa barabara Tanzania TANROADS Mkoani Katavi wamesema, wanafanya mchakato wa kupata wakandarasi wa kujenga miundombinu ya barabara zinazounganisha Mkoa wa Katavi na mikoa jirani.
                                                  
TANROADS


Hayo yamebainishwa na Injinia wa TANROAD Mkoani Katavi  Abdon Malegesi wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Ofisini kwake kuhusu hatua iliyofikwa ya ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuwaondolea adha wasafiri na wasafirishaji mizigo msimu wa masika.
Aidha Malegesi amewataka madereva kuanza kutii sheria za barabarani kwa kutozidisha uzito wa magari yao ili kuzuia uharibifu wa barabara za lami pindi zitakapokamilika.
Nao baadhi  ya Madereva wa magari ya abiria yanayotoka Mpanda Mjini kwenda Vijijini wamesema wanapata  matatizo wakati wa masika ambapo magari yao hukwama kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA