SHULE BINAFSI MPANDA ZAOMBA RUZUKU KUENDESHA SHULE ZAO ILI KUTEKELEZA AGIZO LA SERIKALI
Na.Issack Gerald-MPANDA
WASIMAMIZI wa shule binafsi wameiomba Serikali kuangalia
uwezekano wa Kuzipatia ruzuku za Uendeshaji endapo agizo la ada elekezi
lililotolewa na serikali litapitishwa.
Ombi hilo limetolewa leo na Mkuu wa
shule ya Sekondari Istikama iliyoko Katika Manispaa ya Mpanda Bw,SADICK
ABDALLAH wakati akizungumza na P5
TANZANIA MEDIA ofisini Kwake.
Bw,Abdallah amesema shule binafsi hutumia
gharama kubwa katika uendeshaji wake ikiwemo Kuwalipa Mishahara walimu, hivyo
Kupunguzwa kwa Kiwango cha ada Kinacholipwa na wanafunzi kwa sasa huenda
Kikasababisha kupungua kwa ubora wa elimu unaotolewa na shule hizo.
Aidha Bw,ABDALLAH ameowaomba
wasimamizi wa sekta ya elimu Kuhakikisha wanatoa mwongozo wa Mabadiliko hayo
Kabla ya mwaka wa Masomo wa 2016 ili kutoa nafasi kwao Kujiandaa kwa
utekelezaji huo.
Comments