MTOTO ANAYEDAIWA KUUWAWA NA ASKARI KWA RISASI MLELE AZIKWA
Na.Issack Gerald-MPANDA
Wazazi wakazi wa kijiji cha Kamsisi Wilayani Mlele Mkoani Katavi
wamekubali kuuzika mwili wa mtoto wao Moshi Saleh (17) anayedaiwa kuuwawa kwa
kupigwa risasi za moto na askari wa wanyama pori wa shirika la hifadhi za Taifa
Tanapa Mkoani hapa.
Mwili wa marehemu huyo ulilazimika kuhifadhiwa katika chumba
cha maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa siku tano baada ya wazazi wa
marehemu na wakiwa na wafugaji kukataa kuzika mwili huo mpaka wafahamu chanzo
cha kifo cha mtoto wao.
Mara kadhaa wakazi Mkoani Katavi wamekuwa wakiwalalamikia
askari wa hifadhi za Taifa za wanyama Tanapa kuwafanyia ukatiri.
Hata hivyo waratibu wa haki za binadamu Mkoani Katavi wiki
iliyopita katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu ,walisema vitendendo
vya ukiukwaji wa haki za binadamu havikubaliki Mkoani Katavi.
Comments