BAADHI YA WAMILIKI WA VITUO TIBA ASILIA NA TIBA MBADALA MPANDA WAZUNGUMZIA ZUIO LA SERIKALI KUWEKA MATANGAZO REDIONI
Na.Issack Gerald-MPANDA
Baadhi ya wamiliki wa vituo vya tiba
asilia na Tiba Mbadala Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wamesema kuwa Serikali Ya
Tanzania haijakosea kusitisha utangazaji wa vituo hivyo katika vyombo vya
habari kwa kuwa serikali imesimamia sheria za nchi.
Hayo yamebainishwa na Wamiliki hao
kwa nyakati tofauti, wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA katika Ofisi zao mara baada ya tangazo la
serikali.ALOVERA Miongoni mwa mimea inayotibu baadhi ya magonjwa |
Miononi mwa wamiliki wa vituo vya
tiba mbadala na tiba asilia ni pamoja na Bw.Joseph Kienzi ambaye ni mmiliki wa
kituo cha Jerusalem Herbalist Clinic kilichopo Mjini Mpanda ambaye amewashauri
wamiliki wa vituo kama hivyo kuhakikisha wanapata kibali kutoka Wizara ili
kufanya kazi kwa uhuru.
Kwa Mjibu wa Bw.Joseph amesema
kuwa,vibali vya kutangaza matangazo katika vyombo vy ahabari vimekuwa
vikitolewa na Ofisi za usitawi wa jamii katika Halmashauri za wilayakatika
mikoa husika ambapo amesema kuwa kwa sasa wamiliki wa vituo hivyo wanatakiwa
kupata kibali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Tangazo la serikali kupiga marufuku
utangazaji wa matangazo ya tiba asilia na tiba mbadala katika vyomvo vya habari
lilitangazwa Ijuma iliyopita.
Katika hatua nyingine wamesema kuwa,mpango
huo wa serikali utawabana matapeli wa tiba mbadala na tiba asilia ambao
wamekuwa wakiwatapeli wananchi kwa kuwaibia pesa wakisema kuwa wanawatibu huku
wakiwa hawana kibali cha kufanya matibabu hayo.
Hata hivyo serikali ilitoa siku 14
kwa wamiliki wa vituo vya Tiba Mbadala na tiba asilia wawe wamewasilisha
Wizarani nyaraka za kazi zao ili kupata vibali halali.
Comments