WALAZIMIKA KULA VYAKULA WAKIWA NDANI YA NETI WAKIWAKIMBIA NZI
Moja ya madampo ya taka yanayotoa taka Mpanda mtaa wa Kashaulili |
NA.Meshack Ngumba-Katavi
WAKAZI wa Mtaa wa Kashaulili Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi hulazimika
Kula chakula wakiwa ndani ya Neti kutokana na eneo hilo kuwa na inzi wengi.
Wakizungumza na Mpanda Fm wakazi wa
eneo hilo wamesema wanajifunika neti kutokana na kuwepo kwa Inzi wengi
wanaosabishwa na Jalala la Uchafu lililopo Katikati ya Makazi yao.
Wakazi hao wameongeza kuwa Pamoja na Naibu Waziri wa Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Kufika eneo hilo na Kuagiza Kuondolewa kwa Jalala
hilo bado uongozi wa Manispaa ya Mpanda Umeshindwa Kutekeleza agizo lake.
Ni hivi Karibuni iliyokuwa
halmashauri ya Mji wa Mpanda na sasa Manispaa ilitangazwa kuwa halmashauri ya
Kwanza Nchini inayozingatia Usafi wa Mazingira.
Hata hivyo licha ya Mkuu wa Moa wa
Katavi Dr.Ibrahim Msengi kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali waliopo katika
Halmshauri nne za wilaya kuhamasisha usafi,bado wakazi wa baadhi ya maeneo
hususani Manispaa ya Mpanda wanalalamika kuzagaa kwa takataka katika makazi
yanayowazunguka licha ya kuambiwa kuwa gari la kuzoa taka hizo lipo ili hali
taka hazizolewi.
Comments