ASKARI 15 KATAVI WATUNUKIWA VYETI VYA HESHIMA POLICE FAMILY DAY,WAPANGA MIKAKATI YA KUKOMESHA UHARIFU
Na.Lutakilwa-Lutobeka-Katavi
MAAFISA
15 wa jeshi la polisi mkoani Katavi wametunukiwa vyeti maalum vya utendaji kazi
katika maadhimisho ya siku ya polisi yaliyofanyika leo mjini Mpanda.
Akitunuku
vyeti hivyo Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi kamanda Dhahiri Kidavashali amesema kutokana
na kazi kubwa waliyofanya maafisa hao, kubaini matukio mbalimbali ya kiuharifu
ni bora wakawapa vyeti hivyo kama motisha.
Mbali
na kutunuku vyeti kamanda Kidavashali ametumia sherehe hizo kama sehemu ya
kutathmini kazi zilizofanywa na jeshi kwa mwaka mzima wa 2015 ili kubaini
mafanikio na mapungufu.
Wananchi
waliohudhuria sherehe hizo wameelezea kufurahishwa na utendaji kazi wa jeshi la
polisi kwa mwaka 2015, kwani askari wamekuwa marafiki wa wananchi.
Sherehe
hizo za POLICE DAY ambazo zimefanyika katika viwanja vya polisi Wilayani
Mpanda, zilihusisha michezo mbalimbali ikiwemo riadha na kucheza ngoma.
Hata
hivyo Mkoani Katavi,kumekithiri matatizo ya watu kuuwawa mara kadhaa katika
maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi ambapo watu hawa huuwawa na watu
wasiojulikana lakini pia wengine kuuwawa na wanyama wakali kama simba.
Karibu
watu 10 wamepoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha wengingi wao wakiwa
ni wanaume.
Hata
hivyo jeshi la polisi limesema kuwa,kupitia sherehe hizo,limewasihi wananchi
kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kuwabaini waharifu kabla
ya athari kutokea kwa binadamu.
Maadhimisho
siku ya polisi mkoani katavi yamefanyika
yakiwa na kauli mbiu “UTII WA SHERIA BILA SHURUTI, KATAVI BILA UHARIFU
INAWEZEKANA”.
Comments