MTOTO MIAKA 17 AFA MAJI MPANDA
Na.Issack
Gerald-Mpanda Katavi
MTOTO aliyefahamika
kwa jina la Stanslaus Christopher mwenye umri wa miaka (17) Mkazi wa Mtaa wa
Mpadeco Kata ya Makanyagio Wilayani Mpanda Mkoani Katavi, amekufa maji baada ya
kutumbukia mtoni katika daraja la Kachoma.
Akizungumza na
Mpanda Radio nyumbani kwa Marehemu baba mkubwa wa mtoto huyo, Gaudens Thadeo amesema marehemu alikuwa
anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kabla ya kufikwa na mauti katika tukio hilo
lililotokea jana.
Naye Mwenyekiti
Mtaa wa Mpadeco, Bw. Bernard Nkana, amesema amepata taarifa za msiba huo leo
baada ya kurejea kutoka safarini.
Polisi wa kituo
cha Wilaya ya Mpanda baada ya kupigiwa simu na mashuhuda waliofika katika tukio
hilo walichukua Mwili wa Marehemu na kuupeleka kuuhifadhi katika hospitali ya
Wilaya ya Mpanda kusubiri taratibu za mazishi ambapo taratibu za mazishi
zimefanyika leo.
Huyo ni mtoto wa
pili kufa maji katika familia hiyo ambapo wazazi Mkoani katavi wametakiwa kuwa
na uangalizi wa kutosha kwa watoto wao.
Comments