HIVI KUMBE HALI YA BEI YA DAGAA SUMBAWANGA RUKWA IKO HIVI?
Na.Issack Gerald-Sumbawanga
DAGAA maarufu kama kauzu wanauzwa kwa bei ya juu katika
masoko ya mjini Sumbawanga mkoani Rukwa baada ya kuadimika katika kipindi hiki
cha masika.
Miongoni mwa dagaa wanaouzwa Sumbawanga Mjini Kutoka Rukwa wakivuliwa kutoka Ziwa Tanganyika (PICHA NA.Issack Gerald) |
Kitoweo hiki ambacho pia ni maarufu kama ‘dagaa wa Kigoma’
huvuliwa katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika katika wilaya za Kalambo na Nkasi
mkoani Rukwa.
Imeelezwa kuwa kilo ya dagaa kwa sasa inauzwa kwa Sh 20,000
kutoka Sh 8,000 miezi mitatu iliyopita, ikiwa ni bei ya rejareja baada ya
kuadimika sokoni katika Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa kwa miezi mitatu
mfululizo.
“Msimu wa mvua dagaa hawa wanaadimika sana,isitoshe bidhaa
hii ilikuwa imeadimika kabisa sokoni ambapo sasa bado wanavuliwa kwa taabu sana
huku mahitaji ya walaji wakiwa makubwa,” alisema mchuuzi wa samaki aitwaye
Samweli Kapele.
“Lakini sasa mambo
yamebadilika bei ya dagaa imepaa sana hata tunashindwa kuwatumia ndugu zetu
waishio nje ya mkoa huu kama zawadi kwani kutokana na kipato cha baadhi yetu
tunashindwa kuwanunua,”mmoja wa mkazi wa mjini Sumbawanga aitwaye, Mariam
Kinsukulu alisema.
Chanzo : Wafanyabiashara kutoka Rukwa hadi Katavi.
Comments